Inspector Moses aliingia ofisini kwake na haraka akafungua kabati dogo lilikuwepo ofisini, alipata mshituko nusura moyo wake usimame baada ya kuona kisu cha Maria, “Mungu wangu, nimekwisha……nimekwisha” alisema Moses. Mara simu yake ikaita, haraka aliipokea. “Nadhani umepata ujumbe wangu, nilikwambia muda mrefu uache kunifatilia ila hukusikia, hakuna mtu, jeshi wala serikali yoyote itakayoweza kupambana na...